Nina wasiwasi na mashaka makubwa na maswali mengi sana na majibu yake nahisi yatakuwa ni machache sana.
Tanzania Bara kwa sasa inaundwa na mikoa 21 ya kijiografia lakini nadhani sasa ni wakati ufaao kuwa na mikoa ya kisoka kutoka na idadi ya watu na mahitaji maalum kama asasi za elimu ya juu,majeshi nk.
Unapotaka maendeleo usiwe mvivu wa kubuni na kufikiria na badala kila baada ya kumaliza kazi ya kwanza zingatia changamoto zinazohusika na baadae songa mbele.
Sasa ni wakati ufaao kwa TFF kuondoa dhana ya kuamini kuwa soka ina asili katika mikoa kadhaa na mikoa mingine itabakia kupigapiga makofi tu.Dhana hii ni mbaya sana na inapoteza na kudidimiza vipaji vya wachezaji wetu na kupoteza hazina ya taifa katika medani ya soka.