African Lyon F.C. (http://www.africanlyonfc.com)

Members Login
Username 
 
Password 
    Remember Me  
Post Info TOPIC: YAH:MABADILIKO NI MUHIMU KATIKA MFUMO WA LIGI DARAJA LA KWANZA


Newbie

Status: Offline
Posts: 3
Date:
YAH:MABADILIKO NI MUHIMU KATIKA MFUMO WA LIGI DARAJA LA KWANZA
Permalink   


Nina wasiwasi na mashaka makubwa na maswali mengi sana na majibu yake nahisi yatakuwa ni machache sana.

Tanzania Bara kwa sasa inaundwa na mikoa 21 ya kijiografia lakini nadhani sasa ni wakati ufaao kuwa na mikoa ya kisoka kutoka na idadi ya watu na mahitaji maalum kama asasi za elimu ya juu,majeshi nk.

Unapotaka maendeleo usiwe mvivu wa kubuni na kufikiria na badala kila baada ya kumaliza kazi ya kwanza zingatia changamoto zinazohusika na baadae songa mbele.

Sasa ni wakati ufaao kwa TFF kuondoa  dhana ya kuamini kuwa soka ina asili katika mikoa kadhaa na mikoa mingine itabakia kupigapiga makofi tu.Dhana hii ni mbaya sana na inapoteza na kudidimiza vipaji vya wachezaji wetu na kupoteza hazina ya taifa katika medani ya soka.



__________________
RENjau
Page 1 of 1  sorted by
 
Quick Reply

Please log in to post quick replies.



Create your own FREE Forum
Report Abuse
Powered by ActiveBoard