Elimu ya sekondari na chuo na chuo kikuu ni yenye thamani sana katika maisha binadamu yeyote mwenye tamaa ya maendeleo na nia ya kusonga mbele.Lakini vigumu sana kwa binadamu yeyote kuweza kufikia hapo iwapo hakuna mazingira mazuri katika elimu ya msingi.
Kwa upande wa soka la Tanzania sielewi na sina hakika ni vigezo gani wanazuoni wa soka wanatumia katika kupata timu bora za ligi kuu wakati hakuna udhamini wala promosheni maridhawa katika ligi ya daraja la kwanza.
Huu ni wakati ufaao kwa TFF na wadau wote wa soka kuingia kwenye mchakato wa wa kutafuta wadhamini wa kutosha kwa ajili ya promosheni,kombe na zawadi rasmi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu katika ligi hii.
Udhamini huo uwezeshe katika kubadisha mfumo wa kucheza kwenye vituo na sasa uanze mfumo wa kucheza nyumbani na ugenini ili kuibua na kujenga vipaji vipya pamoja ushabiki kutoka kwa wadau wa soka.
Wakati hayo yakiendelea wadhamini wetu wabadilike na sasa wapite mitaani na magari ya matangazo kila siku ya mechi ili kuwahamasisha wadau na washabiki wahudhurie mechi husika.Wakati mechi huko viwanjani wadhamini waendeshe promosheni za bidhaa na huduma zao kwa wahudhuriaji na kutoa zawadi mbalimbali kwa manufaa ya pande zote zinazohusika.
Wenu kwa staha; Ray Ephraim Ndewingiya Njau Dar es salaam.